MKWAWA: SHUJAA WA UHURU WA WAHEHE DHIDI YA WAKOLONI




UTANGULIZI

Katika historia ya Tanzania, jina la Mkwawa linatambulika kama alama ya ujasiri, uongozi, na mapambano ya kupinga ukoloni. Mkwawa alikuwa chifu wa kabila la Wahehe waliokuwa wakikaa maeneo ya Iringa ya leo. Kupitia mbinu zake za kivita na msimamo wa kutetea uhuru wa watu wake, aliingia kwenye historia kama mmoja wa wapinzani wakubwa wa ukoloni wa Kijerumani.

          Ramani: Kalenga – Iringa (Makao ya Mkwawa)


MAISHA YA AWALI NA UONGOZI

Mkwawa alizaliwa takriban mwaka 1855, akiwa mtoto wa Munyigumba, kiongozi wa Wahehe. Baada ya kifo cha baba yake mwaka 1879, Mkwawa alipambana na changamoto kutoka kwa ndugu na wapinzani wake ili kuchukua uongozi. Mwaka 1880, alifanikiwa kuwa kiongozi mkuu wa Wahehe. Akiwa kiongozi, aliimarisha jeshi na ushawishi mkubwa dhidi ya mataifa ya jirani.


MAPAMBANO DHIDI YA UKOLONI

Mnamo 1891, jeshi la Mkwawa liliwashinda Wajerumani katika Vita vya Lugalo. Aliwaua askari zaidi ya 300 wakiwemo makamanda wao. Ushindi huu ulifanya Mkwawa ajulikane Afrika Mashariki yote kama kiongozi shupavu aliyekataa utawala wa kigeni.


KIFO NA URITHI WA MKWAWA

Baada ya miaka minne ya kujificha na kupambana porini, Mkwawa alikataa kutekwa hai. Tarehe 19 Julai 1898, alijitoa uhai. Fuvu lake lilipelekwa Ujerumani na kurudishwa mwaka 1954. Leo hii, linapatikana katika Makumbusho ya Mkwawa, Kalenga – Iringa

Tazama Video ya Elimu: Historia ya Mkwawa

             GUSA APA KUTAZAMA

Hitimisho

Kumkumbuka Mkwawa ni kutambua thamani ya uhuru. Ni wajibu wetu kama walimu na wanafunzi kuenzi historia hii kwa vizazi vijavyo. Mkwawa ni ishara ya kujivunia utaifa. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni